Mbunge wa Sigor, Peter Lochakapong, amewataka wakazi wa maeneo mbalimbali katika kaunti ya pokot magharibi kuzingatia ushauri unaotolewa na idara ya hali ya hewa kuhusu utabiri wa mvua za El Niño.
Akizungumza na Aperit Fm katika mahojiano ya kipekee, Lochakapong amewaonya wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhamia sehemu salama ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.
Mbunge huyo amesisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua tahadhari mapema, akitaja mafuriko na majanga mengine yaliyoshuhudiwa awali kama sababu ya wakazi kuzingatia tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa hali ya hewa.
APERIT FM,HII NI YETU

