Mahakama kuu ya Malindi imeamua kuwa uchaguzi mkuu wa urais wa Agosti mwaka wa 2027 ni kinyume na sheria, ikisema uchaguzi huo ungepaswa kufanyika Agosti mwaka 2026, kwa mujibu wa Katiba.
Jaji Mugure Thande, amesema tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, itakuwa imekiuka katiba iwapo itafanya uchaguzi wa urais tarehe yoyote baada ya Jumanne ya pili ya Agosti mwaka wa tano.
Mahakama imesema tarehe inayofaa kwa uchaguzi wa urais ni jumanne agosti 11, 2026, badala ya Agosti 10, 2027.
Hata hivyo Jaji Thande, amesitisha utekelezaji wa uwamuzi huo kwa sasa, hivyo uchaguzi wa mwaka 2027 bado haujabatilishwa kiutekelezaji.
Uwamuzi huo umeibua mjadala kuhusu tafsiri ya katiba, kuhusu muda wa muhula wa Rais na tarehe ya uchaguzi mkuu hapa nchini.
Ikumbukwe kuwa wakili Wilis Otieno amekuwa mstari wa mbele kupinga ratiba ya sasa ya uchaguzi, akikariri kuwa uchaguzi mkuu ujao haufai kufanyika mwakani kama ambavyo imeratibiwa.

