You are currently viewing NYOTA! AWAMU YA PILI, BILIONI 6.1 KUTUMIKA

NYOTA! AWAMU YA PILI, BILIONI 6.1 KUTUMIKA

Serikali hapo kesho inatarajiwa kuzindua awamu ya pili ya mpango wa kuwainua vijana kiuchumi wa NYOTA, uku ikilenga kutoa hadi Shilingi elfu 50 kwa kila mmoja wa vijana elfu 222.

Rais William Ruto ataongoza hafla ya utoaji wa fedha hizo Jijini Nairobi, uku Mawaziri wakiongoza shughuli sawa katika vituo vingine 17 kote Nchini.

Naibu wa Rais Profesa Kithure Kindiki, amesema kuwa fedha hizo zitawanufaisha vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 29, uku vijana 70 wakichaguliwa katika kila Kata kote nchini ili kunufaika.

Jumla ya shilingi bilioni 6.1 zinatarajiwa kutumika kufanikisha mpango huo ili kuwawezesha vijana, kuanzisha au kupanua biashara ndogo.