You are currently viewing MBADI ATAKA FEDHA ZA MIKOPO KUELEKEZWA KWA MIRADI YENYE TIJA KWA NCHI

MBADI ATAKA FEDHA ZA MIKOPO KUELEKEZWA KWA MIRADI YENYE TIJA KWA NCHI

Waziri wa fedha , John Mbadi, ameitaka serikali kuhakikisha ukopaji wa fedha za umma unaongozwa na mahitaji halisi ya nchi.

Mbadi amesema kenya imekuwa ikichukua mikopo bila  kutathmini kikamilifu iwapo fedha hizo zinahitajika wakati huo.amesema hali hiyo imesababisha serikali kulipa ada   ambazo zimeidhinishwa kama mikopo japo hazijatumika kwa wakati.

Amesema fedha zinazotumika kulipia ada hizo zingeweza kuelekezwa katika maeneo yenye manufaa zaidi kwa wananchi, yakiwemo miradi ya maendeleo  

Ameelezea umuhimu wa serikali kuboresha mipango ya matumizi ya mikopo ili kuhakikisha fedha zinazokopwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuleta matokeo yanayoonekana.

Aidha  amewataka washirika wa maendeleo kuimarisha mifumo iliyopo ambayo tayari inafanya kazi, badala ya kuanzisha mifumo mipya ambayo inaweza kuongeza gharama na kurudia majukumu yaliyopo.

Amesema ushirikiano huo unapaswa kulenga kuimarisha taasisi na mifumo ya kitaifa ili kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi.

APERIT FM,HII NI YETU