Rais William Ruto amesema kuwa mamlaka ya afya ya jamii (SHA) inaendelea kufanya kazi vizuri na kutoa huduma muhimu kwa wakenya, huku akiwahimiza wananchi wote kujiandikisha kwenye mpango huo ili waweze kunufaika na huduma za afya.
Rais Ruto amesema serikali imefanya maboresho makubwa katika mfumo wa sha ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya bila changamoto zilizokuwepo hapo awali.
Amewahimiza wakenya ambao bado hawajajisajili kufanya hivyo haraka, akisema usajili huo utawawezesha kupata huduma za matibabu kwa urahisi na kuwakinga dhidi ya gharama kubwa za matibabu wanapougua.

