Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, amepinga mpango wowote wa kuwafurusha wageni nchini, akisema serikali inapaswa kushughulikia suala hilo kwa busara na kwa kuzingatia sheria.
Natembeya amesema wageni wanaoishi na kufanya shughuli halali nchini hawapaswi kuchukuliwa kama wahalifu kwa sababu tu ni raia wa mataifa mengine.
Kauli ya gavana Natembeya imechochewa na agizo la rais William Ruto kuhusu biashara ndogo zinazoendeshwa na wageni, huku serikali ikisisitiza kuwa inalenga kuhakikisha wafanyabiashara hao wana vibali na nyaraka zinazohitajika.
Ikumbukwe serikali imetangaza muda wa siku tisini kwa raia wa kigeni wanaoendesha biashara nchini kuwasilisha au kusasisha nyaraka zao, zikiwemo vibali vya kazi na leseni za biashara.
Hatua hiyo kulingana na serikali inalenga kuweka utaratibu katika sekta ya biashara na kuhakikisha sheria za uhamiaji na biashara zinafuatwa, badala ya kuanzisha kampeni ya kuwafukuza wageni wote nchini.
APERIT FM,HII NI YETU

