You are currently viewing KILIMO KUKUMBATIWA KWA UHIFADHI WA CHAKULA NCHINI

KILIMO KUKUMBATIWA KWA UHIFADHI WA CHAKULA NCHINI

Wadau wa sekta ya kilimo nchini wameitaka serikali kuharakisha utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa Kilimohai kwa mabadiliko ya mfumo wa chakula, wakisema ndio suluhu ya kujenga mfumo wa uzalishaji wa chakula unao stahimili athari za mabadiliko ya tabia nchi, na unao linda mazingira.

Wadau hao kutoka serikali za Kaunti na Kitaifa, Mashirika ya Kiraia, Taasisi za utafiti na Elimu ya juu, pamoja na wakulima na wataalamu wa kilimo, wamesema utekelezaji wa mkakati huo utasaidia kuimarisha usalama wa chakula, kurejesha rotuba ya udongo ulioharibika, na kuwajengea wakulima uwezo wa wakukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Maazimio hayo yalipitishwa katika kongamano la Tatu la kitaifa la Kilimo-hai, lililoandiwa na shirika la ‘Pelum Kenya’, kwa ushirikiano na wizara kilimo pamoja na maendeleo ya mifugo.

Washiriki wa kikao hicho wametoa wito kwa serikali kuongeza fedha za kutekeleza mkataba huo, kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, taasisi za utafiti na washirika wa maendeleo pamoja na kuwawezesha wakulima wadogo kupitia mafunzo, huduma za ugani na upatikanaji wa mbegu bora zinazo stahimili mabadiliko ya hali ya anga.

                                                                        APERIT FM HII NIYETU