Rais William Ruto amesema muziki shuleni haupaswi tena kuchukuliwa kama shughuli ya ziada chini ya mfumo wa elimu unaozingatia umahiri, CBE.
Rais amesema muziki sasa ni sehemu ya elimu ya kawaida na serikali inakusudia kuutengea fedha katika bajeti za elimu. Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha vipaji vya wanafunzi na kuwapa fursa ya kukuza uwezo wao katika sanaa na muziki.
Rais Ruto amesema mfumo wa CBE unalenga kutambua na kukuza vipaji mbalimbali vya wanafunzi, huku muziki ukiwa miongoni mwa maeneo yanayoweza kuwasaidia wanafunzi kugundua na kuendeleza vipaji vyao.

