Kenya inaongeza uwekezaji katika mafunzo kwa wakulima, utafiti, uvumbuzi na uongezaji thamani wa mazao, katika juhudi za kujenga sekta ya kilimo inayoweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kilimo ya Kaimosi mwaka huu katika kaunti ya vihiga, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei wamesema marekebisho katika sera na taratibu za kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo yamechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa mahindi na maziwa.
wameongeza kuwa hatua hizo pia zimeanza kurejesha imani miongoni mwa wakulima, huku serikali ikiendelea kuweka mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

