Mbunge wa Turkana ya Kati Emathe Namuar, amewashutumu baadhi ya magavana kwa kutumia uhamisho wa watumishi wa serikali za kaunti kama njia ya kuwaadhibu kisiasa wale wanaodhaniwa kutounga mkono uongozi wao.
Namuar amesema uhamisho wa watumishi unapaswa kufanywa kwa kuzingatia mahitaji ya huduma za umma na maslahi ya watumishi, badala ya kutumiwa kama chombo cha kulipiza kisasi au kushinikiza watumishi kuunga mkono viongozi kisiasa.
Amemtaja gavana wa turkana, Jeremiah Lomorukai, akidai kuwa baadhi ya watumishi wamehamishwa kwa sababu za kisiasa na kupelekwa katika maeneo ambako hayaambatani na vigezo vyao
Kwa mujibu wa Namuar, hali hiyo inaweza kudhoofisha utoaji wa huduma kwa wananchi na utekelezwaji wa majukumu yao ipasavyo.
Amesema watumishi wa umma wanapaswa kulindwa dhidi ya kuhusishwa na siasa za viongozi, kwa kuwa jukumu lao kuu ni kuwahudumia wananchi bila kujali misimamo yao ya kisiasa.

