Chama cha ODM kimeongeza shinikizo la kupewa nafasi ya naibu wa rais katika serikali jumuishi, ODM ikisistiza kuwa nafasi hiyo si ya majadiliano, iwapo kitaunga mkono azma ya Rais William Ruto ya kutetea urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Naibu kiongozi wa chama cha ODM Simba Arati, amesema kwa kuwa Rais Ruto atawania urais kupitia chama cha UDA, basi ODM ndio inapaswa kutoa mgombea wa nafasi ya naibu wa rais.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa junet muhammed.
Ikumbukwe naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki, ameashiria kuwa hayuko tayari kuiacha nafasi hiyo kiurahisi akisema ataendelea kupigania kuwa mgombea mwenza wa rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao 2027.
ODM imetaja baadhi ya viongozi wanao weza kuwania nafasi hiyo, akiwamo Waziri wa yama vya ushirika na biashara ndogondogo Wyclif Oparanya, Waziri wa madini Ali Hassan Joho na gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga.
Hata hivyo chama hicho cha kinasema kipaumbele chake ni kwanza kupata nafasi hiyo, kabla ya kumteua mgombea mwenza wa ruto.
Viongozi wa ODM wanasema mazungumzo rasmi bado hayajaanza, lakini yanatarajiwa kuwekewa msingi katika kikao maalum cha viongozi wa UDA na ODM, kitakacho fanyika wiki ijayo.

