Katika hatua za kuhakikisha wakazi wananufaika na madini inayopatikana kaunti hii gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi Simon Kachapin, mbunge wa Sigor Peter Lochakapongna pamoja na mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto walimtembelea waziri wa Madini, Uchumi wa Baharini, Mhe. Ali Hassan Joho, ofisini kwake kutafuta mbinu mwafaka ya kufaa shughuli hiyo.
Majadiliano yao yalilenga rasilimali kubwa ya madini na ambayo haijatumiwa kwa kiasi kikubwa katika Kaunti ya Pokot Magharibi na fursa zilizopo za kutumia utajiri huu kupitia uchimbaji madini endelevu na uliodhibitiwa vyema. Hii itahakikisha jamii za eneo hili zinanufaika huku pia ikichangia ukuaji wa kaunti yetu na uchumi wa taifa.
Walieleza kujitolea kufanya kazi kwa karibu na serikali ya kitaifa ili kuhakikisha maliasili za kaunti ya Pokot Magharibi zinatumiwa kwa manufaa na ustawi wa wenyeji.