Chama cha kitaifa cha waendeshaji Bodaboda, nacho kimetoa onyo kwa wanachama wake, kutokubali kushiriki shughuli za uhuni.
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho cha waendeshaji bodaboda Kevin Mubadi, amesema kwamba kwa kawaida mara nyingi wanasiasa upenda kuwatumia wanabodaboda kwa ajili ya shughuli hizo za uhuni.
Akizungumza kule Kapsabet katika kaunti ya Nandi, Mubadi amewataka wanabodaboda kususia kabisa vurugu ambazo zinahusiana na wanasiasa, akisema kwa kawaida wanasiasa upenda kuwatumia wahudumu hao kwenye shughuli aina hiyo.
APERIT FM, HII NI YETU

