Zaidi ya wanasiasa 15 wanaodaiwa kuhusishwa na matamshi ya chuki, uwenda wasiruhusiwe kuwania nyadhifa katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Hatua hiyo inafuatia kuundwa kwa kamati ya pamoja inayojumuisha tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI pamoja na afisi ya msajili wa vyama vvya kisiasa.
Msajili mkuu wa vyama nchini John koX lorionokou na mwenyekiti wa kamati ya uwongozi ya jukwa la vyama vya kisiasa Evans Misate, wanasema baadhi ya wanao endelea kufanya kampeni huwenda wasionekane kwenye karatasi za kura, kwa kukosa kufikia viwango vinavyo takiwa na sheria.
Mwenyekiti wa NCIC, Askofu Kepha Omae, anasema kamati hiyo itasimamia uchunguzi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi watakao bainika kuchochea chuki au kutoa matamshi ya uchochezi, uku akisistiza kuwa sheria itafuatwa kikamilifu.
Naye mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethokon, anasema tume hiyo itatangaza rasmi kipindi cha uchaguzi zikiwemo kampeni, baadae mwezi huu. Akiongeza kuwa uchaguzi wa kuaminika hauwezi kufanyika katika mazingira ya chuki na migawanyiko.
Mkurugenzi wa DCI Muhammed Amin, naye amewaonya wanasiasa wanaotoa matamshi ya uchochezi katika mikutano na kwenye mitandao ya kijamii, akisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

