Rais William Ruto ametoa wito wa mageuzi ya mara kwa mara kwenye mfumo wa fedha na utawala wa Kimataifa, akiweka bayana kwamba akiba ya fedha za ndani barani afrika haitumiki ipasavyo kustawisha maendeleo ya bara hilo.
Akizungumza katika mkutano kati ya Kenya na umoja wa ulaya kuhusu mfumo wa kimataifa wa utawala nchini Marekani, rais Ruto amesisitiza umuhimu wa kubadilisha mifumo iliyopo ili kuhakikisha kuwa fedha zinazopatikana ndani ya bara la Afrika zinatumika kwa ufanisi zaidi katika kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo ya mataifa ya Afrika.
Amehimiza haja ya kuwapo na mfumo wa kutatua migogoro inayochipuka baina ya nchi za Afrika katika ngazi ya kimataifa akisema hali hiyo huenda ikazinyima fursa za kimaendeleo na kiuchumi
APERIT FM,HII NI YETU

