You are currently viewing SENETA CHERARGEI AMSUTA WAZIRI MURKOMEN KUHUSIANA NA UTOVU WA USALAMA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

SENETA CHERARGEI AMSUTA WAZIRI MURKOMEN KUHUSIANA NA UTOVU WA USALAMA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

Waziri wa usalama  Kipchumba Murkomen, ameendelea kukosolewa vikali kufuatia matukio ya uhalifu yanayohusisha wizi wa mifugo na machafuko kwenye kaunti za bonde la Kerio na maeneo mengine nchini  na hatua zinazochukuliwa kushughulikia tatizo hilo

Kulingana na seneta wa Nandi Samson Cherargei inashangaza kwamba  washukiwa wanaodaiwa kuhusika na kifo cha padre marehemu Allois Bett bado hawajakamatwa, licha ya serikali kutoa hakikisho mara kadhaa kwamba hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha  amehoji matumizi ya mamilioni ya fedha katika vikao vya jukwaa la usalama, licha ya visa vya  ukosefu wa usalama  kuendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Turkana na pokot magharibi huku pia akipendekeza kuanzishwa kwa hazina maalum ya fidia kwa waathiriwa wa visa hivyo

Cherargei ametaka serikali kutoa maelezo kuhusu matokeo ya vikao hivyo na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha usalama wa wananchi unaboreshwa.

APERIT FM,HII NI YETU