Mwakilishi wa akina mama kaunti ya Pokot Magharibi Rael Kasiwai Aleutum, amesema kuwa kushindwa kwa kenya kwanza katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou ni tukio ambalo halipaswi kutafsiriwa kama mwelekeo wa siasa za uchaguzi mkuu ujao.
Kulingana na Kasiwai serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na kushughulikia mahitaji ya wananchi ili kuimarisha imani yao.
Aidha, ametangaza kuwa ana imani Rais William Ruto atahudumu kwa mihula miwili kamili, akisema viongozi wa muungano huo wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

