Ni afueni kwa wakulima hususan wa mahindi katika eneo la bonde la ufa, baada ya kiangazi cha muda mrefu, hali ambayo imefanya zao hilo kunyauka.
Idara ya hali ya anga nchini, imetabiri mvua kunyesha katika baadhi ya maeneo kwenye eneo hilo kuanzia July 27, huku maeneo mengine wakaazi wakitarajiwa kushuhudia hali ya baridi, mawingi na upepo mkali.
Mvua inatarajiwa kunyesha katika kaunti za nakuru, uasin-gishu, nandi, trans-nzoia na bungoma, kaunti hizo zina wakulima wengi wa mahindi na mazao mengine.
Maeneo mengine ni kakamega, vihiga, nyamira na bomet, sawa na meru na mombasa kule pwani.Katika jiji la nairobi mvua nyepesi huwenda ikanyesha katika baadhi ya maeneo kama vile westlands, mtaa wa dagoreti, mtaa wa kibra na lang’ata uku maeneo mengine yakitarajiwa kuwa na mawingu na vipindi vya jua, joto la juu linatarajiwa kufikia nyuzi 22.Idara hiyo pia imetoa tahadhari ya upepo mkali katika baadhi ya kaunti za kaskazini na kule pwani.
Kaunti zilizoko katika hatari ya mvua kubwa zinazo ambatana na hali ya el-nino, pia zimeshauriwa kuimarisha mipango ya kukabili majanga, uku wataalamu wakionya kuhusu uwezekano wa maafuriko na kuongezeka kwa viwango vya maji katika baadhi ya maziwa nchini.

