Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Pokot Magharibi, Samuel Poghisho, ameendelea kuimarisha kampeni zake za kuwania kiti cha ugavana wa kaunti ya hiyo kuelekea uchaguzi ujao
Poghisho amesema ana imani na ushindi wake akipuuzilia mbali kauli na mbwembwe za kisiasa kutoka kwa wapinzani wake huku akisisitiza kuwa lengo lake kuu si kujibizana kisiasa bali kujenga uhusiano wa karibu na wananchi na kupata uungwaji mkono wa moja kwa moja kutoka mashinani.
Aidha, amewataka wakazi wa Pokot Magharibi kuendelea kushiriki katika mijadala kuhusu mustakabali wa kaunti hiyo, akiahidi kuendeleza sera zinazolenga kuboresha huduma za jamii, kukuza uchumi wa eneo hilo na kuharakisha maendeleo endapo atapewa nafasi ya kuongoza kaunti hiyo mwaka 2027.

