You are currently viewing WENYEJI ELGEIYO MARAKWET WASHAURIWA KUKUMBATIA UPANZI WA VIAZI VITAMU ILI KUKABILI UTAPIAMLO

WENYEJI ELGEIYO MARAKWET WASHAURIWA KUKUMBATIA UPANZI WA VIAZI VITAMU ILI KUKABILI UTAPIAMLO

Katika juhudi za kukabili tatizo la utapia-mlo miongoni mwa watoto wachanga katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet, wakaazi wa Kaunti hiyo wamehimizwa kukumbatia kilimo cha viazi vitamu.

Wito huu umetolewa, huku utafiti ukionyesha kuwa asilimia 22 ya watoto wachanga katika kaunti Hiyo, wameathirika na utapia mlo , mashirika mbalimbali yakijitokeza na kuweka mikakati ya kukabili changamoto hiyo.

Kulingana na Penina Mwogi Afisa katika shirika moja linalo toa msaada wa kijamii, wanashirikiana na mashirika mengine ili kuona kuwa wakulima wanapata mbegu itakayo wawezesha kufanikisha mchakato huo wa kupanda viazi vitamu.