You are currently viewing AFRIKA KUSINI NA TUNISIA, YABANDULIWA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA KOMBE LA DUNIA

AFRIKA KUSINI NA TUNISIA, YABANDULIWA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Afrika Kusini imebanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia.

Afrika Kusini maarufu Bafanabafana, wametupwa nje ya michuano ya kombe la dunia baada ya kufungua bao moja kwa bila dhidi ya Canada jana usiku kwenye mechi ya mchujo wa raundi ya 32 bora.

Mchezaji Stephen Eustaquio aliifungia Canada bao hilo la kipekee na la ushindi, kunako dakika ya 91 zikiwa zimesalia dakika 4 mechi ikamilike.

Hata ivyo Afrika Kusini ni taifa la pili kutoka afrika kubanduliwa kwenye kinyang’anyiro cha kombe la dunia, baada ya tunisia kuondolewa katika hatua ya makundi.

Haya yanajiri kocha wa timu ya taifa la Afrika Kusini hugo broos, alitangaza kujiuzulu dakika chache kabla ya mechi kuanza baada ya mashabiki wa afrika kusini kutishia kukusanya sahihi za kutaka afutwe kazi.

Kuondoka kwa afrika kusini na Tunisia, kunaiacha Afrika na timu 8, ambazo ni Senegal, Algeria, Morocco, Ghana, Misri, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Ivory Coast, pamoja na Cape Verde.

Ikumbukwe tu michuano ya kombe la dunia imeingia raundi ya 32 bora, na leo usiku kutapigwa mechi mbili, saa mbili kamili usiku Brazili itamenyana dhidi ya Japan, kisha baadae saa tano unusu usiku, Ujerumani itakuwa ikikabana koo dhidi ya Paraguay.