You are currently viewing USWISI NA ARGENTINA ZAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

USWISI NA ARGENTINA ZAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

Ruben Vargas wa Uswisi alifunga penalti ya mwisho na kuiwezesha timu yake kuishinda Colombia 4-3 katika mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 bila bao.

Bahati ililalia upande wa Uswisi katika upigaji wa mikwaju ya penalti wakati kipa wao Gregor Kobel alipookoa penalti ya Cucho Hernandez baada ya Davinson Sanchez kugonga mwamba kwa upande wa Colombia. Ingawa Manuel Akanji pia alikosa penalti yake kwa Uswisi, akipiga shuti juu ya mwamba, Ruben Vargas hakufanya kosa, akipiga penalti ya ushindi kwenye kona ya chini.

Akizungumza baada ya pambano hilo kali la kusisimua, Vargas alisema, “Ni vigumu sana kwangu kutambua kile tulichofanikisha leo,” Ninashukuru kwa wakati huu. Ilikuwa mechi ya kushangaza kwangu. Kwa dakika 120 tulijitolea kwa nguvu zote uwanjani. Tulikabiliana na mpinzani hodari, lakini sasa tumeandika historia… Lilikuwa jambo ya kufurahisha sana kwamba nilifanikiwa kufunga penalti ya mwisho.”

Ilikuwa ni huzuni kubwa kwa Colombia, ambao walikuwa wakijaribu kufika robo fainali kwa mara ya pili tu katika historia yao, baada ya hapo awali kufanya hivyo katika Kombe la Dunia la 2014 huko Brazil.