You are currently viewing KENYA YAFUZU KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KWA WASICHANA CHIPUKIZI.

KENYA YAFUZU KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KWA WASICHANA CHIPUKIZI.

Timu ya tafa ya kandanda ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, Junior Starlets wamefuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia.

Kenya imejikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia, baada ya kuipepeta timu ya taifa la Afrika Kusini mabao matatu kwa moja hapo jana.

Ni pambano lililoandaliwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo Jijini Nairobi, na wachezaji Gaudencia Maloba, Brenda Awuor na Elizabeth Alizeba, waliifungia Kenya goli moja kila mmoja.

Hata hivyo Junior Starlets ilishinda mechi ya mkondo wa kwanza magoli mawili kwa bila, na hivyo imefuzu kwa idadi jumla ya mabao matano kwa moja.

Michuano ya Kombe la Dunia kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 itang’oa nanga tarehe 17 Oktoba mwaka huu nchini Morocco.