You are currently viewing UHISPANIA YATINGA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2026

UHISPANIA YATINGA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2026

Uhispania imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia la Fifa 2026 baada ya kuipiga kumbo Ufaransa kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mjini Dallas, Marekani.

Ushindi huo umeiwezesha timu hiyo kufuzu kwa mara ya pili katika historia yake kucheza fainali ya Kombe la Dunia tangu ilipotwaa ubingwa mwaka 2010.

Ushindi huo unaendeleza safari nzuri ya kocha Luis de la Fuente ambaye ameendelea kuiongoza Uhispania katika mafanikio makubwa kwenye mashindano ya kimataifa.

Timu hiyo sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya  Uingereza na Argentina  ili kujua mpinzani wake katika fainali ya Julai 19.

Kwa Upande wa Ufaransa, ndoto ya kucheza fainali ya tatu mfululizo ya Kombe la Dunia imefikia tamati.

Badala yake, Les Bleus sasa watashuka dimbani kuchezea nafasi ya tatu dhidi ya timu itakayopoteza nusu fainali nyingine ijayo.