Kiungo wa Argentina, amesema timu yao ilifanya kazi kubwa kuiwakilisha nchi licha ya kadi nyekundu na matukio mbalimbali yaliyozua mjadala.
Kungo wa Argentina Enzo Fernandez amesema timu yake iliwakilisha nchi kwa njia bora zaidi katika michuano ya Kombe la Dunia, licha ya kadi nyekundu aliyopewa katika fainali na matukio kadhaa yaliyoibua utata katika kampeni yao.
Kutokana na matukio hayo FIFA ilianzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya wachezaji wa Argentina. Timu hiyo pia ilizua mjadala baada ya kugeuza mgongo wakati Uhispania ikikabidhiwa medali na kombe, na kwa kuonyesha bango la madai ya umiliki wa Visiwa vya Falkland baada ya mechi ya nusu fainali.
Kupitia Instagram, Fernández amewashukuru mashabiki na kusisitiza kuwa kuivaa jezi ya Argentina ni heshima kubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Wakati huo huo, kipa Emiliano Martínez amesema anatafakari mustakabali wake katika timu ya taifa baada ya kushindwa kutetea ubingwa wa dunia.

