Kiungo wa zamani wa Manchester United na Juventus, Paul Pogba, ameachana na klabu ya Monaco baada ya msimu mmoja tu.
Hatua hii inaweweza kuashiria mwisho wa maisha yake ya soka barani Ulaya.
Pogba, mwenye miaka 33, amekuwa akipambana kurejea kwenye kiwango cha juu tangu kutumikia adhabu ya dawa za kuongeza nguvu, huku akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Monaco imesema imeamuachilia Pogba kwani malengo waliyoweka “yamefikiwa kwa sehemu tu”, hivyo kusitisha mkataba wake uliotarajiwa kuendelea hadi 2027. Pogba alicheza dakika 115 tu msimu uliopita na kwa sasa anauguza jeraha la paja.
Licha ya changamoto, klabu imemsifu kwa uongozi na uzoefu alioutoa kwa wachezaji wenzake. Pogba, mshindi wa Kombe la Dunia 2018 , sasa anahusishwa na klabu kadhaa za ligi ya Marekani.
APERIT FM, HII NI YETU

