Rais wa chama cha wafanyibiashara na viwanda Erick Rutto, amesema sekta ya biashara nchini inaunga mkono dira ya baada ya ruwaza ya mwaka wa 2030, akieleza kuwa mpango huo unatoa matumaini mapya kuhusu mwelekeo wa uchumi wa nchi.
Rutto amesisitiza kuwa wafanyabiashara wana hamu ya kuona malengo ya maendeleo ya kenya yakitekelezwa kwa kasi ili wananchi waanze kunufaika na matokeo ya juhudi zao mapema.
Akitoa hoja yake katika mazungumzo kuhusu ajenda ya kitaifa ya maendeleo baada ya vision 2030, dkt. Rutto ameitaka serikali, sekta binafsi na wadau wengine kufanya kazi kwa pamoja katika kuandaa na kutekeleza dira hiyo.
Aidha amesisitiza umuhimu wa mfumo unaoongozwa na wananchi na unaowashirikisha wadau mbalimbali katika kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

