GARI AINA YA TOYOTA HILUX YATUMBUKIA MTARONI PKOPOCH

Gari aina ya Toyota Hilux limepoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni katika eneo la pkopoch, kando ya barabara kuu ya Makutano–Kacheliba, kaunti ya Pokot Magharibi.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo    gari hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi kabla ya kugonga matuta   na kupoteza mwelekeo.

Wamewataka madereva   kuwa makini na waangalifu zaidi wanapotumia barabara ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.

APERIT FM,HII NI YETU