Seneta wa kaunti ya Baringo Vincent Chemitei amesema viongozi wa kisiasa kutoka eneo la bonde la ufa wameafikiana kwa kauli moja kumteua gavana wa nandi, stephen sang, kuongoza kampeni za Rais William Ruto katika eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Chemitei amesema uamuzi huo unatokana na makubaliano ya viongozi wa eneo hilo ya kuunganisha nguvu zao ili kuhakikisha rais ruto anapata uungwaji mkono mkubwa kutoka rift valley.
Seneta huyo pia amewataka wakazi wa Rift Valley kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kama wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Hata hivyo, suala la nani hasa atakuwa na jukumu la kuratibu kampeni za uda na washirika wake katika maeneo mbalimbali ya Rift Valley linaendelea kuwa sehemu ya mjadala wa kisiasa katika eneo hilo.

