You are currently viewing JUHUDI ZAIDI ZAPASWA KUELEKEZWA MIPAKANI ASEMA GAVANA KACHAPIN

JUHUDI ZAIDI ZAPASWA KUELEKEZWA MIPAKANI ASEMA GAVANA KACHAPIN

Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi, Simon Kachapin, ametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usalama katika mpaka wa jamii za Pokot na Turkana.

Amesema kuendelea kwa mapigano na uhasama katika maeneo ya mipakani  yanaathiri maisha ya wananchi, shughuli za kiuchumi pamoja na maendeleo ya maeneo hayo.

Ametoa wito kwa serikali kupitia wizara ya usalama kuhakikisha silaha zote zinazomilikiwa na raia kinyume na sheria zinatwaliwa

Wakati huo uo  Kachapin amewataka viongozi kuepuka kuingiza siasa katika mzozo huo, akisema hali ya usalama inahitaji juhudi za pamoja ili kulinda maisha ya wananchi na mali zao.

Amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuweka mbele maslahi ya wananchi na kushirikiana na vyombo vya usalama pamoja na jamii za eneo hilo kutafuta suluhu ya kudumu ya mzozo huo.

APERIT FM,HIINI YETU

 ‎