You are currently viewing KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAANGAZIA MIKAKATI YA MAPEMA KABLA YA ELNINO

KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAANGAZIA MIKAKATI YA MAPEMA KABLA YA ELNINO

Kaunti ya Pokot Magharibi imeanza kuweka mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa mwezi ujao.

Akizungumza mjini kapenguria wakati wa kikao na wadau mbalimbali ,naibu gavana wa kaunti hiyo, Robert Komole, amewataka wadau mbalimbali kushirikiana katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kabla ya mvua hizo kuanza.

Amesema maandalizi ya mapema na hamasisho kutoka kwa idara tofauti ikiwamo vyombo vya habari  yatasaidia kuokoa maisha na mali, kinyume na  zilizoshuhudiwa  miaka iliyopita.

Komole ametoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kuelekeza nguvu na rasilimali zao katika kuimarisha utayari wa jamii, akisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana kwa ufanisi na changamoto zozote zitakazoweza kujitokeza.
‎Wakati huo uo, Komole amehimiza kuwepo kwa mikakati ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua, huku wenyeji wakipewa mbegu bora ili waweze kuzalisha chakula wakati wa msimu huo wa mvua.

Amesema hatua hizo zitasaidia jamii kutumia vyema mvua zinazotarajiwa, kuimarisha uzalishaji wa chakula na kukabiliana na changamoto ya uhaba wa chakula katika siku zijazo.

APERIT FM,HII NI YETU