Seneta wa kaunti ya Turkana, James Lomenen, ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka katika kuangazia changamoto za ukosefu wa usalama unaoendelea katika mpaka wa Pokot Magharibi na Turkana
Lomenen amesema wakazi wa maeneo ya mpakani wameendelea kukabiliwa na matukio ya wizi wa mifugo, mashambulizi ya mara kwa mara na kuwasababisha kuhama makaazi yao kutokana na ukosefu wa usalama.
Ametoa wito wa kupatikana kwa suluhisho la kudumu badala ya hatua za muda mfupi ambazo, amesema, hazijatatua kikamilifu changamoto hiyo.
Amesema serikali inapaswa kuimarisha usalama katika maeneo yaliyoathiriwa, huku ikiweka mikakati ya kukabiliana na wizi wa mifugo na migogoro kati ya jamii za Turkana na Pokot.
Wakati huo uo amesisitiza umuhimu wa serikali kuangazia hatua za muda mrefu zitakazosaidia kurejesha amani, kuwawezesha wananchi kurudi katika maeneo yao na kulinda maisha pamoja na mali zao.
APERIT FM ,HII NI YETU

