You are currently viewing MAKAAZI YA LAMIN YAMAL YAVAMIWA NA MAJAMBAZI

MAKAAZI YA LAMIN YAMAL YAVAMIWA NA MAJAMBAZI

Watu wasiojulikana walivamia makaazi ya mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania Lamin Yamal muda mfupi baada ya nyota huyo kuipatia ushindi timu yake katika nusu fainali ya kombe la dunia

Polisi nchini Uhispania imesema watu wasiojulikana walijaribu kuvamia nyumba ya mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania, Lamine Yamal, saa chache baada ya kuisaidia nchi yake kutinga fainali ya Kombe la Dunia kwa kuibwaga Ufaransa.

Kwa mujibu ya polisi wa jimbo la Catalonia, watu wawili waliokuwa wameficha nyuso zao walipanda ukuta wa nyumba hiyo iliyoko Esplugues de Llobregat, nje kidogo ya mji wa Barcelona, lakini walikimbia baada ya kugunduliwa na walinzi binafsi.

Gazeti la La Vanguardia limeripoti kuwa nyumba hiyo iliwahi kumilikiwa na nyota wa zamani wa Barcelona Gerard Piqué na aliyekuwa mpenzi wake, Shakira.

Tukio hilo lilitokea alfajiri ya Jumatano, muda mfupi baada ya Uhispania kuifunga Ufaransa mabao 2-0 mjini Arlington, Texas na kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2026.