Mahakama ya Nakuru imemuondolea mashtaka Seneta wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, katika kesi iliyohusu mpango wa ufadhili wa masomo wa Finland wenye thamani ya takriban shilingi bilioni 1.1.
Katika uamuzi uliotolewa hapo jana mahakama ilisema kuwa Mandago hakupatikana na hatia kuhusiana na mashtaka yaliyokuwa yanamkabili katika suala hilo.
Akizungumza mara baada ya kuachiwa huru, Mandago alisema kuwa sasa ni jukumu la serikali ya kaunti ya uasin gishu kushughulikia suala la mpango huo na kuhakikisha wazazi walioathirika wanarejeshewa fedha zao.
Amesisitiza kuwa familia nyingi zilipata hasara kutokana na mpango huo na kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua za haraka ili kutatua changamoto zilizowakumba waathiriwa na kurejesha imani ya wananchi.

