Mbunge wa Tiaty, William Kamket, amemtaka Spika wa bunge la kitaifa, Moses Wetang’ula, kumpa waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi amri ya kufika mbele ya bunge ili kutoa maelezo kuhusu matumizi na usimamizi wa hazina ya usawazishaji
Kamket amesema kuna haja ya bunge kuchunguza kwa kina namna fedha hizo zinavyosimamiwa, akidai kuwa kwa sasa mfuko huo unatumika visivyo na baadhi ya magavana.
Amesisitiza kuwa hazina hiyo ilianzishwa kwa lengo la kusaidia maeneo yaliyotengwa na ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za maendeleo kwa muda mrefu,na kwamba kucheleweshwa au kutotumika ipasavyo kwa fedha hizo kunaathiri wananchi wanaotegemea miradi ya maendeleo katika maeneo yao, ikiwemo miradi ya maji, barabara, afya na huduma nyingine muhimu.
Kamket amemtaka spika wetang’ula kuhakikisha waziri wa hazina anafika mbele ya bunge na kujibu maswali yanayohusu fedha hizo, ikiwemo namna zinavyotolewa, zinavyosimamiwa na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha zinawafikia wananchi walengwa.
mbunge huyo pia amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma, akisema viongozi wa kitaifa na wa kaunti wanapaswa kuhakikisha rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya wananchi zinatumika ipasavyo.
APERIT FM,HII NI YETU

