Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, ameendelea kuitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, kuchunguza madai ya usajili wa raia wa Uganda kama wapigakura nchini
Akizungumza katika eneo la Chepchoina, Natembeya amesema raia wa kigeni hawafai kuruhusiwa kushiriki katika uchaguzi nchini
Ametaka IEBC kuhakikisha kuwa mchakato wa usajili wa wapigakura katika maeneo ya mpakani unafanyika kwa mujibu wa sheria.
Natembeya pia amesema amefanya mazungumzo na vyombo vya usalama kuhusu udhibiti wa mipaka, akisisitiza haja ya kuhakikisha kuwa raia wa uganda hawaingii nchini bila sababu halali wakati wa msimu wa uchaguzi.
APERIT FM,HII NI YETU

