You are currently viewing ZIARA ZA RAIS UGHAIBUNI ZAFUNGUA FURSA KWA VIJANA

ZIARA ZA RAIS UGHAIBUNI ZAFUNGUA FURSA KWA VIJANA

‎Katibu  wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, John  Tanui, amesema ziara za kiserikali za Rais William Samoei Ruto katika mataifa mbalimbali zimefungua fursa nyingi kwa vijana wa Kenya, hususan katika sekta ya teknolojia, ubunifu na ajira za kidijitali.

‎Tanui amesema kupitia ushirikiano ulioanzishwa kati ya Kenya na mataifa mbalimbali, vijana wengi wamepata nafasi za mafunzo, ajira za mtandaoni, uwekezaji katika sekta ya teknolojia na programu za kukuza ujuzi wa kidijitali.

‎Aidha, amesisitiza kuwa Wizara ya habari mawasiliano na UCHUMI dijitali inaendelea kutekeleza miradi ya upanuzi wa miundombinu ya intaneti, vituo vya kidijitali na programu za mafunzo ya ujuzi wa teknolojia nchini kote ili kuwawezesha vijana kushindana katika soko la ajira la kimataifa.

‎Tanui amewahimiza vijana kutumia fursa hizo kwa kujifunza teknolojia mpya, ubunifu na ujasiriamali wa kidijitali, akisema hatua hiyo itachangia kupunguza ukosefu wa ajira na kuimarisha uchumi wa taifa.