You are currently viewing MBUNGE WA TIATY WILIAM KAMKET AENDELEA KUSHINIKIZA MFUMO WA DEMOKRASIA YA MAAFIKIANO KATI YA ENEO BUNGE LAKE NA BARINGO KASKAZINI

MBUNGE WA TIATY WILIAM KAMKET AENDELEA KUSHINIKIZA MFUMO WA DEMOKRASIA YA MAAFIKIANO KATI YA ENEO BUNGE LAKE NA BARINGO KASKAZINI

Mbunge wa Tiaty, William Kamket, amependekeza mfumo wa demokrasia ya maafikiano kati ya maeneo ya tiaty na baringo kaskazini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kamket amesema Tiaty iko tayari kumuunga mkono mgombea wa ugavana kutoka Baringo Kaskazini huku  akipendekeza kuwa eneo hilo  limuunge mkono mgombea kutoka tiaty katika nafasi ya uwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Baringo.

Kwa mujibu wa Kamket, mpango huo unalenga kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kudumisha umoja, na kupunguza ushindani unaoweza kugawanya viongozi na wananchi wa kaunti hiyo kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027.