You are currently viewing WAFANYIBIASHARA WA SINA NA TAPACH WAPATA MWANGA BAADA YA KUZINDULIWA KWA MRADI WA UMEME

WAFANYIBIASHARA WA SINA NA TAPACH WAPATA MWANGA BAADA YA KUZINDULIWA KWA MRADI WA UMEME

Wakazi wa vituo vya biashara vya Tapach na Sina sasa wanatarajiwa kunufaika na usalama ulioimarishwa baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa taa za barabarani.

Akizungumza baada ya uzinduzi  huo gavana Simon Kachapin amesema mradi huo, ambao ulikuwa sehemu ya ahadi ya kuboresha miundombinu katika maeneo ya biashara, unalenga kuongeza usalama, kuwezesha wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao hadi nyakati za   usiku, pamoja na kuhakikisha mazingira salama kwa wafanyibiashara

Ameongeza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuimarisha miundombinu inayokidhi mahitaji ya wananchi, kukuza shughuli za kiuchumi na kuharakisha maendeleo endelevu katika maeneo mbalimbali ya kaunti.

Amewahimiza wananchi   kutunza miundombinu hiyo ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa manufaa ya jamii kwa muda mrefu.