You are currently viewing GAVANA KACHAPIN ATOA WITO KWA WENYEJI NA VIONGOZI KUKUMBATIA UJIO WA CHUO KIKUU POKOT MAGHARIBI

GAVANA KACHAPIN ATOA WITO KWA WENYEJI NA VIONGOZI KUKUMBATIA UJIO WA CHUO KIKUU POKOT MAGHARIBI

Gavana wa kaunti ya pokot magharibi, simon kachapin, amesema mipango ya kuanzisha chuo kikuu katika kaunti hiyo inaendelea vyema, akisisitiza kuwa mradi huo ni muhimu katika kuboresha upatikanaji wa elimu ya juu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya eneo hilo.

Gavana kachapin amesema kuwa kuanzishwa kwa chuo kikuu kutawapa vijana wa pokot magharibi na maeneo jirani nafasi ya kupata elimu ya kiwango cha juu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu, akiongeza kuwa taasisi hiyo itachangia utafiti, ubunifu, uundaji wa nafasi za ajira na ukuaji wa biashara katika kaunti hiyo.

Wakati huo uo, kachapin amewakosoa viongozi wa kisiasa wanaopinga mpango huo, akisema kuwa siasa hazipaswi kuzuia miradi ya maendeleo inayowanufaisha wananchi. Amesema viongozi wanapaswa kuweka maslahi ya wananchi mbele badala ya tofauti za kisiasa, akionya kuwa upinzani usio na msingi unaweza kuchelewesha maendeleo muhimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.