You are currently viewing WAKULIMA KUPATA AFUENI KWA PEMBEJEO, BAADA YA KIANGAZI KIREFU

WAKULIMA KUPATA AFUENI KWA PEMBEJEO, BAADA YA KIANGAZI KIREFU

Rais William Ruto ameahidi kupunguza bei ya mbolea ili kuwasaidia wakulima kurejea mashambani wakati wa msimu wa mvua za buli, zinazo tarajiwa kuanza mwezi huu hadi Disemba, katika juhudi za kuongeza uzalishaji wa chakula kufuatia hasara kubwa iliyo sababishwa na ukosefu wa mvua.

Akizungumza katika kaunti ya Uasin Gishu, rais Ruto amesema wakulIma wengi, walipoteza mazao yao mashambani kutokana na kosefu wa mvua, akiwahimiza kutumia msimu ujao wa mvua, kufanya upanzi upya ili kuhakikisha taifa hili linapata chakula cha kutosha.

Rais amesema kuanzia mkwa ujao serikali itapunguza pembejeo za kilimo, ili kuwapa wakulima fursa ya kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza uhaba wa chakula nchini.

Akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua za kuwawezesha wakulima kuzalisha chakula.

Mwaka huu ukosefu wa mvua uliatthiri uzalishaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya nchi hasa Bonde la Ufa, Kusini mwa Bonde la Ufa, Magharibi ya Kenya na sehemu za Mashariki.

Maeneo hayo ni kaunti za Uasin-Gishu, Trans-Nzoia, Nandi, Nakuru, Bomet, Narok, eneo la Elgeiyo Marakwet, Kericho, Laikipia, Nyandarua, Makueni, Kitui, Machakos, Embu, Tharaka Nithi pamoja na kaunti ya Meru.

Hali hiyo ilisababisha kupungua kwa uzalishaji wa mazao muhimu kama vile mahindi, maharagwe na mazao mengine ya chakula hatua iliyozua wasiwasi kuhusu utosholezo wa chakula na mapato ya wakulima.