You are currently viewing  WAZIRI OGAMBA ATETEA MFUMO MPYA WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU

 WAZIRI OGAMBA ATETEA MFUMO MPYA WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU

Waziri wa elimu, Migos Ogamba, amesema mfumo mpya unaopendekezwa wa ufadhili wa elimu ya juu utaanza kutekelezwa baada ya kuidhinishwa na bunge.

Ogamba amesema wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu mwezi septemba wataandikishwa chini ya mfumo wa sasa  

Ameongeza kuwa wanafunzi hao watahamia katika mfumo mpya baada ya mswada uliowasilishwa bungeni  kupitishwa na kuwa sheria.

Kulingana naye mageuzi hayo yanalenga kubadilisha mfumo wa serikali wa kuzingatia kipato cha familia, na badala yake kuelekeza uwekezaji moja kwa moja kwa wanafunzi na mustakabali wao.