Mbunge wa Mogotio Kiborek Reuben amesema hashangazwi na madai ya idara ya upelelezi wa jinai, DCI, kuhusu mawasiliano yanayodaiwa kuwepo kati ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na maafisa wa polisi wanaotajwa katika uchunguzi huo.
Kiborek amemtaja Gachagua kama mnafiki, akisema madai hayo yanapaswa kuchunguzwa kwa kina na kwamba, iwapo ushahidi utathibitisha kuhusika kwake, anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kukamatwa.
Kulingana naye Gachagua amekuwa akihusishwa na matukio mbalimbali ya uhuni na matamshi yanayoweza kugawanywa taifa

