WANASIASA WAMEENDELEA KUHIMIZWA KUEPUKA UHUNI KWENYE SIASA ZAO

Seneta wa Nandi, samson Cherargei, amewataka wanasiasa nchini kuepuka matumizi ya makundi ya vijana   maarufu kama goons kwenye mikutano ya kisiasa ili kuzua vurugu

‎Cherargei amesema viongozi wa kisiasa wanapaswa kuhimiza umoja, ushirikiano na amani, badala ya kutumia vitisho na migawanyiko katika harakati zao za kisiasa.

‎Amesema Kenya inahitaji utulivu na mshikamano wa kitaifa ili kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali, akisisitiza umuhimu wa viongozi kushirikiana katika kufanikisha ajenda ya Vision 2060 ya Rais William Samoei Ruto.

‎Ameongeza Kuwa  tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa chanzo cha migawanyiko au machafuko, bali ziwe fursa ya viongozi kujadili sera na masuala yanayogusa maisha ya wananchi.

‎wakati huo uo amewahimiza wanasiasa kuweka mbele maslahi ya taifa na kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga Kenya yenye amani, umoja na maendeleo endelevu.