You are currently viewing ASKOFU KOSGEI AHIMIZA SIASA KOMAVU NA MARIDHIANO KUELEKEA MWAKA WA 2027

ASKOFU KOSGEI AHIMIZA SIASA KOMAVU NA MARIDHIANO KUELEKEA MWAKA WA 2027

 Mbunge Mteule askofu Jackson Kosgei amewataka wanasiasa nchini kubadilisha mtazamo wao kuhusu siasa na kuanza kuweka mbele maslahi ya taifa, umoja na mshikamano wa Wakenya, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

‎Kosgei amewahimiza viongozi kuacha siasa za ukabila, migawanyiko na mashindano yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi, akisisitiza umuhimu wa kujenga siasa zinazowaleta Wakenya pamoja.

‎Amesema viongozi wanapaswa kutumia majukwaa ya kisiasa kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano, badala ya kuchochea tofauti miongoni mwa wananchi.

‎Mbunge huyo amesisitiza kuwa siasa za kitaifa zinapaswa kuwa na ajenda inayolenga kuboresha maisha ya wananchi wote, bila kujali maeneo wanakotoka au misimamo yao ya kisiasa.

‎Kosgei amewataka Wakenya na viongozi wao kujifunza kutokana na changamoto za kisiasa zilizopita na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2027 unafanyika kwa amani, heshima na mshikamano wa kitaifa