You are currently viewing MALAWI NA CAMEROON ZATINGA NUSU FAINALI WAFCON

MALAWI NA CAMEROON ZATINGA NUSU FAINALI WAFCON

Malawi na Cameroon zimefanikiwa kuingia nusu fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, WAFCON, na kufuzu kushiriki Kombe la Dunia.

Cameroon ilitinga nusu fainali baada ya kuichapa mabingwa watetezi Nigeria kwa bao 1-0 huku Malawi iliyoshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ikiilaza Ghana kwa mabao 2-1.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nigeria ambao pia ni mabingwa mara 10 wa WAFCON kushindwa kuingia nusu fainali, ambayo itashuhudia Cameroon ikichuana na wenyeji Morocco siku ya Jumatano.

Cameroon ilikuwa imecheza na Nigeria mara 13 hapo awali kwenye Kombe la Afrika la Wanawake na ilishinda mara moja tu kabla ya mechi ya Jumapili huko Casablanca.

                                                                                                           APERIT FM, HII NI YETU