Lionel Messi na timu yake ya Argentina atakabana koo na Misri kutafuta tiketi ya robo fainali ya Kombe la Dunia. Nyota huyo analenga kuendeleza umahiri wake katika mbio za kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa mashindano hayo.
Mabingwa hao watetezi wanakutana na taifa hilo la Afrika, linaloongozwa na Mohamed Salah, mjini Atlanta ambapo mshindi atakutana na Uswisi au Colombia katika nusu fainali.
Messi mwenye umri wa miaka 39, nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe na Erling Haaland wa Norway wote wana mabao saba kila mmoja. Lionel Messi na Mbappe pia wako katika kinyang’anyiro cha taji la mfungaji bora katika historia yaKombe la Dunia, ambapo Muargentina huyo anaongoza na 20 na Mbappe akiwa na 19.
Wakati huo huo, Uswisi na Colombia zitavaana mjini Vancouver, Canada, katika mechi kati ya timu mbili ambazo hazijapoteza mchezo kwenye mashindano haya. Colombia wamefungwa bao moja tu mpaka sasa na wana safu kali ya ushambulizi ya Luis Diaz na mshindi wa Kiatu cha Dhahabu mwaka wa 2014 James Rodriguez. Uswisi hawajatinga robo fainali tangu mwaka wa 1954, walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo.

