You are currently viewing IEBC KUWEKA MIKAKATI YA FEDHA ZA KAMPENI KABLA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA UJAO

IEBC KUWEKA MIKAKATI YA FEDHA ZA KAMPENI KABLA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA UJAO

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, imependekeza kiwango cha juu cha matumizi ya fedha za kampeni kwa wagombea wa Urais kuwa shilingi Bilioni 4.44, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Katika mapendekezo hayo yaliyomo kwenye rasimu ya kanuni za ufadhili wa kampeni za uchaguzi, vyama vya kisiasa vitaruhusiwa kutumia hadi shilingi bilioni 17.7 katika shughuli za kampeni.

IEBC imesema mapendekezo hayo yatawasilishwa kwa umma kwa maoni kabla ya kuwasilishwa bungeni.

Tume iyo pia imeitaka Bunge kupitisha marekebisho hayo kabla ya mwisho wa mwezi Agosti mwaka huu, ili kuipa muda wa kutosha wa kujianda kwa uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa IEBC hatua iyo inalenga kutekeleza kikamilifu sheria ya ufadhili wa kampeni za uchaguzi na kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa ya haki kwa kudhibiti matumizi ya fedha katika nafasi zote za uwongozi ambazo zinagombewa.