You are currently viewing MISHAHARA KWA WAFINYKAZI WA UMMA KUFANYIWA NYONGEZA KWANZIA AGOSTI MOSI

MISHAHARA KWA WAFINYKAZI WA UMMA KUFANYIWA NYONGEZA KWANZIA AGOSTI MOSI

Maelfu ya wafanyikazi wa umma wanatarajiwa kuanza kupokea nyongeza ya mishahara kuanzia Agosti mosi mwaka huu, baada ya waziri wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku, kutangaza utekelezwaji wa ongezeko hilo.

Akizungumza mjini Londiani katika kaunti ya Kericho, Ruku amesema nyongeza hiyo iliyoagizwa na Rais William Ruto, itawanufaisha watumishi wote wa umma nchini.

Kwa mujibu wa Ruku, marekebisho hayo hayatahusu mishahara ya msingi pekee, bali pia yatahusisha marupurupu mbali mbali yanayolipwa kwa wafayikazi wa serikali.

Waziri huyo pia ameeleza taasisi zote za serikali kuhamishia mara moja mifumo yao ya malipo kwenye mfumo wa serikali wa taarifa za rasilimali watu maarufu kama Government Human Resources Information System.

Kwa mujibu wa Ruku, hatua hiyo itahakikisha kuwa ongezeko la mishahara linawanufaisha watumishi halali wa umma pekee, uku ikisaidia kuwatambua na kuwaondoa wafanyikazi hewa katika orodha ya malipo ya serikali.

Amesisitiza kuwa serikali imejizatiti kuboresha ustawi wa watumishi wa umma, uku ikiendelea kuimarisha uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa rasilimali watu serikalini.