You are currently viewing KENYA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUIMARISHA MIFUMO YAKE YA AFYA ASEMA MAMA WA TAIFA 

KENYA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUIMARISHA MIFUMO YAKE YA AFYA ASEMA MAMA WA TAIFA 

Mkewe    rais mama Rachel Ruto amesisitiza dhamira ya kenya ya kuimarisha mifumo ya afya nchini, huku akieleza umuhimu wa kuhakikisha wanawake na watoto wachanga wanapata huduma bora za afya.

Amesema kila mwanamke anapaswa kupata huduma za afya kwa wakati, hasa wakati wa ujauzito, kujifungua na kipindi cha baada ya kujifungua. Amesema hatua hizo ni muhimu katika kuhakikisha afya na usalama wa mama na mtoto.

Aidha amesisitiza haja ya kuweka mifumo madhubuti ya afya itakayowezesha kina mama na watoto kupata huduma muhimu bila vikwazo. Ameeleza kuwa afya ya mama na mtoto ni msingi muhimu wa kujenga jamii yenye afya na taifa lenye nguvu.

  Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, wahudumu wa afya, mashirika na jamii katika kuhakikisha huduma za afya ya mama na mtoto zinapatikana na kufikiwa na kila mwanamke, bila kujali mahali anapoishi.

APERIT FM,HII NI YETU